Tarehe ya mwisho ya kupokea kazi zitakazo shiriki kwenye shindano la Ajru-Risaalah

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya shindano la (Ajru-Risalah) la filamu fupi, imesema kuwa siku ya mwisho ya kupokea kazi zitakazo shiriki ni tarehe kumi na tano mwezi huu.

Kamati ya maandalizi ya shindano ilianza kupokea kazi tangu tarehe moja ya mwezi huu wa nne.

Shindano hili linaandaliwa na kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kufundisha misingi ya kibinaadamu iliyopo katika uislamu, na madhumuni matukufu yaliyopo katika mafundisho ya Mtume na watu wanyumbani kwake (a.s), kwa lengo la kusahihisha picha mbaya inayopewa uislamu, kupitia vipande vifupi vya video zinazo fundisha misingi ya kuishi kwa amani, na kuweka misingi ya kuaminiana baina ya waumini wa Dini tofauti.

Kwa maelezo zaidi bonyeza link ifuatayo:

https://alkafeel.net/news/index?id=12495
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: