Sayyid Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na kuzungumza mambo mengi muhimu

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na kukutana na rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu pamoja na rais wa chuo na baadhi ya wakufunzi.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Sayyid Swafi amefuatana na katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake, amezungumza mambo mengi yanayo gawika sehemu tatu, miongoni mwa aliyo sema ni:

Kwanza: Ametahadharisha athari za mazingira ya sasa yasisababishe kushuka kwa kiwango cha elimu, taifa letu linaishi katika hali maarufu chini ya janga la virusi vya Korona, janga hili linavyo chukua muda mrefu litaathiri sekta ya malezi na elimu, kama zinavyo athirika sekta zingine, inahofiwa kushuka kwa viwango vya elimu na watu kufeli –kutokana na janga la Korona- kwani mfumo wa maisha umebadilika, usije ukabadili pia kiwango cha elimu na kuharibu ubora wa elimu na viwango vya ufaulu.

Bila shaka mazingira tunayo ishi ni maarufu kwa kila muiraq, lakini pia tuliwahi kuishi na kupita salama katika mazingira kama haya miaka ya vita vya muda mrefu vilivyo fanya watu wengi wakashidwa kusoma, na wakaacha kuona umuhimu wa elimu, wakawa watu wa kukata tamaa katika kila jambo, kwa sababu vita huvunja moyo, viliathiri sana umma huu.

Na leo janga hili limechukua muda mrefu, hatutaki iwe ni sababu ya kuvunjika moyo, na kizuwizi cha mafanikio, hatutaki vijana wetu wawe na mtazamo mbaya, au waanze kuvunjika moyo na kuacha kufanya juhudi, hii ni sawa na fitna ya kuwazuwia kutafuta elimu na kuharibu malengo yao, tunatakiwa kuzinduka na kuangalia hatari ya uvivu unao anza kuenea katika maisha, matokeo ya uvivu ni mabaya huharibu kila jambo.

Mheshimiwa alikua amesha tuma ujumbe ulio sisitiza kupambana na mazingira ya sasa, akatahadharisha athari za kuacha kufanya kazi ndogo na kubwa, akatoa wito wa kutumia janga hili kama fursa ya kuleta maendeleo na sababu ya kushajihisha utafutaji zaidi wa elimu, Mheshimiwa akasema kuwa uongozi mkuu wa taasisi na uongozi mkuu wa chuo unatakiwa uonyeshe njia, kwa kutumia wakuu wa vitengo, wakufunzi, watumishi na wanafunzi katika kuondoa tatizo la uzembe, na kuhakikisha watu wanafanya kazi, tunatakiwa kutumia watumishi wetu na kudumisha mawasiliano nao, pamoja na kufungua milango kwa kila mtu anayetaka kufanya jambo zuri, taasisi zenye mamlaka zitengeneze mazingira ya kuwasaidia vijana wetu, na kuwawezesha kutekeleza miradi yao, kuwe na aina ya kuwapongeza watu wanaostahiki kupongezwa, ionekane tofauti kati ya mtu anayefanya jambo muhimu na mtu wa kawaida.

Pili: Akasisitiza umuhimu wa kuwa na mpango kati wa wazi unao eleweka, ili watu wautekeleze kwa kutumia mbinu za kielimu, na kuboresha njia za malezi na ufundishaji, na kutengeneza mazingira ya ushindani, husaidia mtu kufanya kila anacho weza, na kuweka vyenzo wezeshi za kufanya tafiti za kielimu, na kuwapa msaada wa hali na mali ili kuweza kupambana na hali ya sasa.

Tatu: Kujikamilisha kielimu, kijamii na kujitegemea, Mheshimiwa amefafanua kuwa (malezi, elimu na afya) vina umuhimu wa pekee, hiyo ni miradi ya kutumikia jamii, inahitaji msaada wa mali ili kuwezesha utendaji wake, lakini sio mbaya kama miradi hiyo ikiweza kujiendesha yenyewe, mradi wowote ukiweza kujiendesha wenyewe hua umejitengenezea msingi madhubuti wa mafanikio.

Lakini miradi yetu ya malezi na elimu pamoja na afya inaweza kusaidiana pia, kila mmoja ukasaidiwa na mwingine katika kuhudumia jamii, ukizingatia kuwa sheria ya kuanzishwa kwake iraruhusu jambo hilo, na sisi tunapenda kuona jambo hilo linatokea.

Bila shaka misaada inayotolewa na Atabatu Abbasiyya katika miradi hii inatakiwa maendeleo yaonekane kwenye sekta ya malezi na elimu yanayo lingana na misaada hiyo, kila msaada unapokua mkubwa ndivyo matokeo yanatakiwa kuwa makubwa zaidi, tunasubiri kuona matunda makubwa ya miradi hii na maendeleo mazuri.

Mwisho wa kikao Mheshimiwa akasema, tunatakiwa kuisha katika matarajio haya, hatutakiwi kusahau kumtegemea Mwenyezi Mungu, kumsahau Mwenyezi Mungu ni sababu ya kufeli, Hakika Mola mtukufu huwa pamoja na mja wake pale mja atakapokua pamoja nae, mazingira yamebadilika kabisa, yajayo ni mazuri kwa juhudi za taifa na raia wake, kisha Mheshimiwa akaomba Mwenyezi Mungu atuondolee janga hili na atupe amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: