Chuo kikuu cha Al-Ameed pamoja na wizara ya elimu wanatafuta namna ya kuboresha elimu

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimepokea ugeni kutoka wizara ya elimu ya juu, uliokuja kujadili pamoja nao njia za kuboresha elimu.

Ugeni huo umeongozwa na Dokta A’amir Salim Amiir, wamekagua majengo ya chuo pamoja na kumbi za madarasa na vifaa vya kufundishia, sambamba na vyumba maalum vinavyo tumika katika kufundisha kwa njia ya mtandao.

Wakajadili maendeleo ya kielimu na njia za kuboresha elimu, zilizo pasishwa na wizara tangu lilipozuka janga la virusi vya Korona, na athari yake katika sekta zote za maisha ikiwemo sekta ya elimu hapa nchini.

Mwisho wa ziara yao, wakapongeza kiwango cha elimu ya juu kinacho tolewa na chuo kikuu cha Al-Ameed, na kazi kubwa inayo fanywa na wakufunzi ikiwa ni pamoja na kutoa mitihani kwa njia ya mtandao, aidha wamesifu mafanikio makubwa ya chuo hicho yaliyo patikana ndani ya muda mfupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: