Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake, imekusudia kufanya kila jambo linalo weza kumsaidia zaairu, miongoni mwa mambo waliyo fanya katika kuhakikisha hilo wameandaa muongozo wa zaairu, kiongozi wa idara hiyo Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Hakika idara inaendelea kufanya kazi ya kuhudumia jamii ya wanawake, tumelipa umuhimu mkubwa swala la kujibu maswali yanayo ulizwa mara nyingi na mazuwaru, hususan yanayo husu uwepo wao ndani ya majengo matukufu ya Ataba”.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa machapisho yetu kuhusu swala hilo ni (muongozo wa zaairu), linalo jibu maswali mengi ya kifiqihi, kuhusu kuingia kwa mazuwaru wa kike katika malalo za Ataba na mazaru tukufu”.
Akasema: “Maswali na majibu yameandikwa kwa njia nyepesi na rahisi kueleweka kwa kila msichana anayekuja kufanya ziara pamoja na kutofautiana kwa viwango vya elimu”.
Akabainisha kuwa: “Vitabu vya muongozo wa zaairu vinapatikana ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu sehemu zinapowekwa Quráni na vitabu vya dua, ili iwe rahisi kusomwa na kila mtu wakati wa kufanya ziara ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Tambua kuwa idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake imefungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na hufanya harakati mbalimbali za kielimu, kitamaduni na Quráni kipindi chote cha mwaka.