Atabatu Abbasiyya imepokea ugeni kutoka chuo kikuu cha Karkhi na rais wake amesisitiza kuwepo juhudi kubwa ya kuhudumia wanafunzi wa vyuo.

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Karkhi Dokta Thaamir Abdul-Ameer Hassan amesema kuwa “Hakika Atabatu Abbasiyya inafanya kazi kubwa kwa wanafunzi wa chuo, katika kuboresha utamaduni na elimu, tutaimarisha ushirikiano kwa ajili ya kuboresha huduma za kielimu, na nitatoa wito kwa vyuo vikuu vinufaike na harakati zinazo fanywa na Ataba tukufu”.

Hayo yamesemwa wakati wa kuhitimisha ratiba iliyo andaliwa na idara ya uhusiano wa vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya, mbele ya zaidi ya wageni (80) kutoka chuo kikuu cha Karkhi wakiwa ni wanafunzi na walimu.

Ustadh Hassan amesema: “Hakika tumepata mapokezi mazuri sana kutoka kwa wasimamizi wa ratiba hii, yatufaa kujivunia na kupongeza mapokezi tuliyopewa, sisi kama wanafunzi na walimu tunatambua kuwa kuna kazi kubwa inafanyika inayo lenga kutumikia taifa na raia wake, tunatarajia ushirikiano uendelee baina yetu, jambo hili tutalijadili katika vikao vya chuo, shukrani za pekee ziende kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuandaa fursa hii”.

Msemaji wa idara hiyo Ustadh Mustwafa Kaadhwimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ratiba hii ni sehemu ya kongamano la kitamaduni kwa wanafunzi wa chuo kikuu chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, wiki hii tumepokea ugeni kutoka chuo kikuu cha Karkhi katika mkoa wa Bagdad, baada ya kuwapokea na kuwaambia kwa ufupi kuhusu malengo ya kongamano hili, tulianza kutekeleza ratiba iliyodumu kwa muda wa siku tano, yenye vipengele vingi na tulianza kwa kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja”.

Akaongeza kuwa: “Tumeunda kamati ya wataalam kwa ajili ya mashamba ya Saaqi ya tende, imeangalia aina ya mitende na ardhi pamoja na vifaa vya shamba, kisha tukatembelea sehemu za kihistoria katika mkoa mtukufu wa Karbala, tumetembelea pia ngome ya kijani na uwanja wa ndege, kisha tukaenda katika jengo la kibiashara la Afaaf kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali, na mji wa Sayyid Auswiyaa ambao upo chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu”.

Akaendelea kusema: “Utamaduni tumeupa umuhimu mkubwa, tumetoa mihadhara mingi kwa wanafunzi ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu, wazungumzaji walikua ni Mheshimiwa Sayyid Saami Albadri na Ustadh Jassaam Saidi pamoja na raisi wa chuo, wameongelea kuhusu jinsi ya kutunza heshima katika changamoto mbalimbali na namna ya kumfanya mwanafunzi kuwa kiigizo chema katika jamii, sambamba na kuwafundisha uzalendo”.

Wanafunzi na walimu wao wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuwapa nafasi hii waliyosema, imewasaidia kupata walichokua wanakitafuta, wakaomba ratiba hii irudiwe tena siku zijazo na ihusishe vyuo vikuu vingi zaidi kwa ajili ya kuzinufaisha na ratiba hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: