Opresheni kubwa ya usafi na upuliziaji dawa yashuhudiwa katika jengo la Shekh Kuleini

Maoni katika picha
Watumishi wa jengo la Shekh Kuleini (r.a) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya opresheni kubwa ya kusafisha na kupuliza dawa sehemu zote zinazo tumika kutolea huduma, na kuziweka tayali kwa ajili ya shughuli yeyote itakayo fanywa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kiongozi wa utumishi anayesimamia kazi hiyo Ustadh Haidari Arabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wetu wanafanya kazi kila siku katika jengo hilo lililopo barabara ya (Bagdad / Karbala), lakini katika msimu wa ziara utendaji wao huongezeka zaidi, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hulipa umuhimu maalum jengo hilo, ikiwa ni pamoja na wakati wa mwezi wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya usafi iliyo shuhudiwa kwa muda wa siku kadhaa, imehusisha kupiga deki barabara kubwa na ndogo zinazo elekekea kwenye jengo hilo, pamoja na vyoo, jiko, stoo, kumbi na sehemu za bustani, sambamba na maeneo ya jirani na jengo hilo”.

Akabainisha: “Sehemu yote ya jengo yenye ukubwa wa mita (7500) imesafishwa, na kupulizwa dawa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kuweka mazingira salama kiafya”.

Akaendelea kusema: “Wamesafisha pia sehemu ya bustani pamoja na kuchambulia miti na kuondoa iliyo haribika pamoja na kupanda mipya”.

Kumbuka kuwa jengo la Shekh Kuleini (r.a) ni sehemu muhimu inayohudumia mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lipo umbali wa kilometa (17) takriban, lilijengwa rasmi kwa ajili ya kuhudumia watu wanaokuja kufanya ziara katika Ataba mbili takatifu, pamoja na kuwa sehemu ya kufanyia shughuli mbalimbali za Ataba tukufu, kwani linakumbi muwafaka kwa ajili ya shughuli.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: