Miswala (1000) imetandikwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya kimemaliza kutandika ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mazulia (1000) ya kifahari kwa ajili ya kupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, kazi hiyo imefanywa pamoja na kutandika miswala katika eneo takatifu linalo zunguka kaburi na kuweka mapambo yanayo endana na utakatifu wa eneo hilo.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya kutandika mazulia mapya hufanywa kila baada muda fulani, kulingana na ratiba na hali ya mazulia yaliyo tandikwa, baada ya kumaliza ziara ya mwezi kumi na tano Shabani na katika kujiandaa kuupokea mwezi wa Ramadhani, watumishi wa kitengo chetu kwa kushirikiana na idara ya masayyid pamoja na watumishi wa kujitolea kutoka vitengo vingine wametandika mazulia mapya ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya kutandika mazulia hutanguliwa na kazi ya kutandua mazulia ya zamani na kuyapeleka sehemu ya kuoshea mazulia, kwa ajili ya kuoshwa na kwenda kutumiwa sehemu zingine, halafu hupiga deki na kupuliza dawa ya kujikinga na maambukizi kisha hutandikwa mazulia mapya kama ilivyo pangwa”.

Akaendelea kusema: “Mazulia mapya yaliyo tandikwa yamefika (1000), mazulia (750) yanaukubwa wa (mt5 x 3) na yanarangi nyekundu, yametandikwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu, na mazulia (250) yanaukubwa wa (mt2 x 3) yametandikwa kwenye eneo linalo zunguka malalo takatifu na ndio yalikua ya kwanza kutandikwa”.

Kumbuka kuwa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kina majukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni kutandua na kutandika mazulia kila baada ya muda fulani, kwa ajili ya kulinda uzuri wa haram tukufu na kudumisha muonekano wa kiroho anaopata mtu anayekuja kufanya ziara katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: