Idara ya Quráni inatoa wito wa kushiriki kwenye usomaji wa Quráni wa wanawake katika mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya tablighi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa wito wa kushiriki katika visomo vya Quráni vya wanawake vitakavyo anza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa anuani isemayo (kuimarisha nyoyo), maalum kwa wanawake wanaonufaika na ratiba ya idara ya Quráni tu.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na kukaribia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuzingatia usomaji wa Quráni katika mwezi wa Quráni, chini ya ratiba iliyo andaliwa kwa ajili ya mwezi huu, tutaendesha kisomo cha Quráni kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (google meet) kwa muda wa saa moja kila siku, pamoja na masomo mengine yanayo saidia kuimarisha Imani katika Quráni, sambamba na kunufaika na mazingira haya kwa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu, ukizingatia kuwa tunaishi katika kipindi cha janga la Korona linalo zuwia kufanya visomo vya watu kuhudhuria moja kwa moja kutokana na masharti ya afya”.

Tambua kuwa idara tajwa inafanya harakati kwa njia ya mtandao za usomaji wa wa Quráni na mashindano tofauti kipindi chote cha mwaka, na chini ya masomo mbalimbali ya Fiqhi na Quráni yanayo saidia kumjenga mwanamke katika usomaji sahihi, wasichana zaidi ya (1500) wamenufaika na ratiba hii ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: