Mwezi mosi Ramadhani kwa mujibu wa matarajio ya ofisi ya Sayyid Sistani

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani, inatarajia kuonekana mwezi muandamo wa Ramadhani jioni ya siku ya Jumanne (30 Shabani 1442h) sawa na tarehe (13 Aprili 2021m) katika anga la mji mtukufu wa Najafu wakati wa kuzama jua saa (12:30) jioni, mwezi utaonekana wazi ukiwa juu, na siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani inatarajiwa kuwa Jumatano ya tarehe (14 Aprili 2021m), hayo yapo katika jeduali la mwezi muandamo wa Ramadhani tukufu katika mwaka (1442h) sawa na mwaka (2021h) lililopa katika toghuti ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu, mwezi utakuwa juu kwa kiwango cha daraja (14) na (16), muda wa kubakia katika anga baada ya kuzama jua ni saa moja (1) na dakika (12) na kiwango cha mwanga ni (% 1.70).

Katika jeduali hilo inaonyesha kuwa mwezi (29 Shabani) hauwezekani mwezi kuonekana kwa macho moja kwa moja.

Kumbuka kuwa taarifa hii sio fatwa ya Marjaa Dini mkuu, bali ni matarajio ya wanaanga, hakika kuthibiti kwa mwezi muandamo kunategemea kuandama kwa mwezi kisheria, kwa hiyo tunawamba waislamu wote waangalie mwezi muandamo na kama wakiuona watoe taarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: