Kitengo cha Dini kimetangaza ratiba ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza ratiba ya mwezi wa Ramadhani, yenye vipengele vya kitamaduni na kidini vinavyo endana na mazingira ya mwezi huu mtukufu, pamoja na kuzingatia masharti ya afya.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekh Aadil Wakili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumezowea kuandaa ratiba yenye vipendele vingi kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani, lakini kutokana na janga la Korona, huu ni mwaka wa pili ratiba yetu inakua na mambo machache yenye manufaa makubwa”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya mwaka huu inavipengele vya Aqida, Fiqhi pamoja na uhuishaji wa matukio yaliyo tokea ndani ya mwezi huu, kama vile kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) na siku za Lailatul-Qadri”.

Akabainisha kuwa: “Baadhi ya ratiba zitahudhuriwa na washiriki kwa sharti la kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi, huku ratiba zingine zikifanywa kwa njia ya mtandao, kama vile masomo ya Fiqhi na kitamaduni yatarushwa kwenye:

  • - Dirisha maalum la picha za video.
  • - Mtandao maalum wa kitengo cha Dini.
  • - Mitandao ya mawasiliano ya kijamii kupitia kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel katika link ifuatayo: https://www.facebook.com/ALKafeel.Art.Production/

Na youtube: https://youtu.be/nf1KP4Ie3fs.”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba itatekelezwa pamoja na mambo mengine, kama vile kujibu maswali yatakayo ulizwa mubashara au kwa njia ya mtandao kupitia dirisha la maswali, au kwa kupiga simu moja kwa moja kwenye kitengo cha Dini kupitia namba zifuatazo: (009647706020688) na (009647803857576) na utajibiwa na mmoja wa watumishi wa kitengo cha Dini”.

Kumbuka kuwa lengo la kuandaa ratiba hii ni kunufaika na mwezi huu mtukufu, kwa kupata mafundisho ya Dini kama tulivyo husiwa na Mtume pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), na kutumia vizuri msimu wa ibada na dua na kumuomba Mwenyezi Mungu akubali matendo yetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: