Maoni katika picha
Miongoni mwa maneno hayo ni:
Karibu karibu karibu
Karibu ewe mwezi wa Ramadhani
Karibu ewe mwezi wa kukombolewa na moto karibu
Karibu ewe mwezi wa twaa na msamaha
Karibu ewe mwezi wa wema na ihsaan
Karibu karibu karibu
Karibu elfu moja kwa kipenzi mwema baina ya walimwengu
Karibu elfu moja kwa mliwazaji wa kudumu kwa walimwengu
Ewe muokozi wa watu sisi tunaogelea katika giza…
Ukaribisho huo ni kitendo cha kurithi, kimekuwa kikifanywa kila unapokaribia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, watu wa Karbala wamezowea kusikia ukaribisho huo kana tangazo la kuanza kwa funga, katika zama hizi umekua ukitolewa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, wasomaji wa Ataba mbili takatifu husoma tenzi na kaswida nzuri zinazo andaa nyoyo za waumini, waliopo katika malalo mbili takatifu ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), au katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na maeneo yanayo zunguka sehemu hiyo, au wale wanao angalia katika luninga zao.