Kitengo cha malezi na elimu kimepokea ugeni kutoka wizara ya ulinzi

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumanne ya jana, kimepokea ugeni kutoka ofisi ya wizara ya ulinzi/ kituo cha mafunzo na maendeleo.

Ugeni huo umekuja kuangalia mfumo unaotumika kuboresha utendaji wa idara, hususan katika sekta ya shule za Al-Ameed.

Ugeni umetembelea baadhi ya shule na kukagua mfumo wa idara na utekelezaji wake.

Wamepongeza na kufurahishwa na mfumo unaotumiwa na idara ya malezi na elimu ya juu, na wamesema kuwa wamenufaika na ziara hii na watajitahidi kupeleka mfumo huo katika taasisi zao.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimepata mafanikio makubwa katika sekta ya kuboresha huduma zake, uzowefu wake umekua ukiigwa na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: