Kituo cha ibun Sina cha mafunzo ya kimtandao: Chuo kikuu cha Alkafeel ni sawa na vyuo vingine vya kimataifa duniani

Maoni katika picha
Mkuu wa kituo cha ibun Sina cha masomo ya kimtandao katika chuo kikuu cha Basra Dokta Adi Bashiri Issa amesema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel ni sawa na vyuo vingine vya kimataifa duniani, kinasifa nzuri ya majengo na madarasa pamoja na maabara zinazo tumia teknolojia ya kisasa.

Wakati wa ziara yake katika chuo kikuu cha Alkafeel akiwa na ujumbe alio fuatana nao amesema: “Tumekuja chuo kikuu cha Alkafeel kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati yake na chuo kikuu cha Basra, na kunufaika na uzowefu wa pande zote mbili, pamoja na maswala ya teknolojia”.

Baada ya ziara hiyo Issa ametoa wito kwa vyuo vikuu vya serikali na binafsi vifuate nyayo zake, akasema kuwa chuo hiki ni kitovu cha elimu na inafaa kujifunia.

Kumbuka kuwa chuo Kikuu cha Alkafeel katika mji mtukufu wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya juhudi kubwa ya kujiendeleza kiutaratibu na kielimu na kuhakikisha kinakua kitovu cha tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: