Kuanza kisomo cha Quráni katika mwezi wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, jioni ya jana Jumatano ambayo ilikua siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ya mwaka (1442h) sawa na (14 Aprili 2021m), imeanza kisomo cha Quráni kitakacho endelea hadi mwisho wa mwezi, ndani ya Sardabu ya Imamu Hassan (a.s) katika ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufuata masharti ya afya na usalama.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadu Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Usomaji wa Quráni ni moja ya harakati za Maahadi katika mwezi wa Ramadhani, zamani tulikua tunasomea ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kushiriki wasomoji maarufu wa Quráni pamoja na mazuwaru, huu ni mwaka wa pili mfululizo tunasoma katika utaratibu huu kwa sababu ya kuwepo kwa janga la virusi vya Korona, na kufuata maelekezo ya idara ya afya inayo pambana na maambukizi ya virusi hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Pamoja na mazingira ya sasa tunafanya kisomo kinacho hudhuriwa na idadi maalum ya wasomaji pamoja na idadi maalum ya watumishi wa malalo takatifu, aidha tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kisomo hiki kitafanywa kila siku kuanzia saa kumi na moja Alasiri na kurushwa na vyombo vya habari, kupitia masafa ya bure iliyotengenezwa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, kila siku tunasoma juzuu moja la Quráni na tunatumia muda wa saa moja”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya vikao mbalimbali vya usomaji wa Quráni ndani ya kipindi cha mwaka mzima kwa kuzingatia hukumu za usomaji na tajwidi vikiwemo vikao hivi, kutokana na mazingira ya mwaka huu tumetosheka na aina hii ya usomaji kama ilivyokua mwaka jana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: