Mwezi ambao mmeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Hakika Allah (s.w.t) ameweka nyakati maalum kwa waja wake zinazotakiwa wafanye ibada kwa wingi, na wajikurubishe kwake kwa kufanya dhikri na ibada mbalimbali, miongoni mwa nyakati hizo ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa quráni, kheri, baraka na dua, hakika huu ni mwezi wa kuswali, mwezi wa kufanya wema, mwezi wa kuachwa huru na moto yeyote atakae tubia na kurudi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Tunatakiwa kufanya ibada kwa wingi katika mwezi huu mtukufu, imepokewa katika khutuba ya Mtume (s.a.w.w) aliyotoa wakati wa kuukaribisha mwezi wa Ramadhani, kama ilivyo simuliwa na Huru Al-Aamiliy katika kitabu cha Wasaailu-Shia (juzu 10/ ukurasa 313) Mtume (s.a.w.w) anasema:

Hakika mnaijiwa na mwezi wa Mwenyezi Mungu na baraka, rehema na maghafira, mwezi mbora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, siku zake ni bora zaidi, usiku wake ni mbora zaidi, saa zake ni bora zaidi, ni mwezi ambao mmeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu, naye ndiyo mkirimu wenu, pumzi zenu mnaandikiwa thawabu za tasbihi na usingizi wenu ni ibada, ibada zenu zinakubaliwa, dua zenu zinajibiwa, muombeni Mwenyezi Mungu Mola wenu kwa nia za kweli, na nyoyo safi, akuwezesheni kufunga na kusoma kitabu chake.

(Hakika muovu zaidi ni yule atakaekosa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu, njaa na kiu (funga) iwakumbushe njaa na kiu ya siku ya kiama, toweni sadaka kwa masikini wenu na mafakiri, heshimuni wakubwa wenu na muwahurumie wadogo zenu, ungeni undugu wenu na mlinde ndimi zenu, fumbeni macho katika vitu ambavyo sio halali kuviangalia, wala msisikilize yasiyo halali kusikilizwa, hurumieni mayatima wa watu nao watahurumia mayatima wenu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu dhambi zenu na muinue mikono wakati wa kumuomba…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: