Ziara na ibada maalum zinafanywa kwa niaba ndani ya mwezi wa Ramadhani kila siku

Maoni katika picha
Idara ya ufundi taaluma na mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ratiba maalum ya idada na ziara kwa niaba katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kupitia ukurasa wake wa ziara kwa jiaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, kwa ajili ya kumfanyia ziara kila atakaeshindwa kuja kufanya ziara kutokana na mazingira ya janga la virusi vya Korona au kwa sababu nyingine yeyote, kwa kushirikiana na idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema kuwa: “Hakika mtandao wa kimataifa Alkafeel kila msimu wa kiibada, pamoja na mwezi wa Ramadhani huandaa ratiba maalum ya kiibada kupitia ziara kwa niaba, yenye vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kila siku hufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Kushiriki katika usomaji wa Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya.
  • - Kufanya baadhi ya ibada maalum za mwezi huu, ikiwemo kusoma dua ya Iftitaahi na zinginezo.
  • - Kusoma ziara maalum ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake katika mji wa Madina jirani na kaburi lake takatifu.
  • - Kufanya ibada maalum za siku za Lailatul-Qadri.
  • - Kufanya ziara maalum ya kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake kwenye malalo yake takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Ibada hizo huhitimishwa kwa kufanya ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku na mcha wa Iddi”.

Akafafanua kuwa: “Mtu yeyote aliye ndani au nje ya Iraq anaweza kutumia fursa hii kwa kusajili jina lake kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba: http://alkafeel.net/zyara”.

Tambuka kuwa kufanya ziara kwa niaba ni moja ya huduma muhimu inayo tolewa na mtandao wa Alkafeel kupitia dirisha la ziara kwa niaba, mwaka jana jumla ya ziara kwa niaba milioni moja laki moja na elfu sitini na nane na mia sita na nane (1,168,608) zilifanywa kwa niaba ya watu kutoka nchi mbalimbali duniani, kupitia mtandao wa (kiarabu, kiengereza, kifarsi, kituruki, kifaransa, Kiswahili, kijerumani, kiurudu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: