Diyala na Dhiqaar zimezindua mashindano ya kitaifa ya usomaji wa Quráni tukufu kwa vikundi

Maoni katika picha
Jumatano ya jana mwezi mosi Ramadhani (1442h) sawa na tarehe (14 Aprili 2021m) imeanza awamu ya saba ya shindano la Quráni la kitaifa, lililo andaliwa na kituo cha kuandaa wasomaji, kuna jumla ya vikundi (20) vinavyo shiriki kwenye shindano hili kutoka mikoa tofauti ya Iraq, siku ya kwanza ya shindano hili vimeshiriki vikundi vya Diyala na Dhiqaar, vikafuata vikundi vya Misaani na Karkuuk katika juzu la pili, ndani ya Sardabu ya Imamu Hassan (a.s), katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya utekelezaji wa kanuni za kujikinga na maambukizi.

Kiongozi wa kituo cha miradi ya Quráni katika Maahadi ya Quráni tukufu Sayyid Hassanaini Halo amesema kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani, zilizo andaliwa rasmi kwa ajili ya mwezi huu mtukufu, shindano linafanywa katika mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona, janga hilo limesababisha mashindano haya kufanywa katika utaratibu huu, wasomaji wa Quráni kutoka mikoa tofauti wamekusanyika katika ukumbi wa haram ya mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kila kikundi kina watu watatu (msomaji, haafidhu na mfasiri), kila mmoja katika watatu hao anamaswali yanayo muhusu, kuna maswali ya usomaji, kuhifadhi na tafsiri”.

Akafafanua kuwa: “Shindano linafanywa chini ya majaji walio babea katika hukumu za usomaji, sauti na naghma, tafsiri, mada na kusimama, kuanza na hifdhu”.

Kumbuka kuwa shindano hili ni sehemu ya ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani inayo endeshwa na Maahadi ya Quráni tukufu, kwa ushiriki wa vikundi kutoka mikoa tofauti ya Iraq, shindano linahusu hukumu za usomaji, kuhifadhi na tafsiri, linarushwa moja kwa moja na vyomba tofauti vya habari kupitia masafa ya bure iliyo tengenezwa na kituo cha uandaaji wa vipindi Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: