Ukarabati mkubwa unafanywa katika moja ya sehemu za kuhudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Idara ya ukarabati katika jengo la Shekh Kuleini inafanya matengenezo makubwa ya vifaa vya umeme kila sehemu ya jengo hilo, kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa kiangazi pamoja na shughuli za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa idara hiyo Sayyid Muslim Swahibu Alyasiri: “Ukarabati huu hufanywa mwanzoni mwa kila msimu, hukarabati vifaa vyote vya umeme kama vile viyoyozi, feni na taa”.

Akaongeza: “Watumishi wa idara hii wanaratiba maalum ya utendaji ndani ya mwaka mzima kulingana na mahitaji, kuna matengenezo makubwa ambayo hufanywa mwanzoni mwa kila msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kwa ajili ya kuweka tayali sehemu zote zinazo tumika kutoa huduma, hivyo tumekarabati sehemu zote za jengo pamoja na vyoo na kubadilisha vifaa vilivyo haribika na kuweka vipya”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunakazi zingine kama vile kupamba jengo na kuweka taa za kuwakawaka ndani na nje, kwa ajili ya kuweka muonekano mzuri, taa hizo hufungwa kwenye miti, kuta, nguzo kwa namna nzuri ya kupendeza”.

Kumbuka kuwa jengo la Shekh Kuleini ni sehemu muhimu ya kutoa huduma kwa mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lipo umbali wa kilometa (17) takriban kutoka katika malalo mbili takatifu, lilijengwa kwa ajili ya kuhudumia watu wanaokuja kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu, pamoja na kuwa na shughuli zingine ambazo hufanywa na Ataba tukufu, kwani linakumbi nzuri zinazofaa kwa shughuli mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: