Mradi wa jengo la ofisi za Atabatu Abbasiyya upo katika hatua ya kukagua mifumo yake

Maoni katika picha
Jengo la ofisi za vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu lipo katika hatua ya mwisho ya ukaguzi wa mifumo yake, pamoja na kuandaa baadhi ya maeneo yake, na kuwa tayali kukabidhiwa ndani ya muda uliopangwa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema: “Huu ni mradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, utasaidia kuongeza uwanja wa kuhudumia mazuwaru ndani ya haram tukufu, hivi sasa mradi upo katika hatua ya mwisho”.

Akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inatilia umuhimu mkubwa miradi inayolenga kuhudumia mazuwaru moja kwa moja, kwa kuweka mazingira muwafaka ya kiroho wakati wa kufanya ziara, haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia upanuzi ulio ongeza uwezo wa kupokea mazuwaru wengi zaidi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa sardabu na mradi wa upauwaji”.

Akaendelea kusema: “Katika kukamilisha mradi tuliotaja ndipo likaja wazo la mradi wa jengo la vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, ili kutafuta nafasi zaidi ndani ya haram tukufu, ikiwa ni pamoja na kuweka ufanisi wa utendaji katika muundo wa idara za Atabatu Abbasiyya”.

Akasisitiza kuwa: “Ujenzi umefanywa kwa ubora mkubwa, sambamba na kuwa na mambo muhimu, kuna mitambo inayo saidia utendaji, kuna mfumo wa kutoa tahadhari, mfumo wa zimamoto, mfumo wa viyoyozi, mfumo wa ulinzi na mfumbo wa intanet, pamoja na eneo la vyoo vya umma”.

Kumbuka kuwa mradi umejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m1395) jengo lina ghorofa kumi, tabaka la chini linaukubwa wa mita (1100) litatumika kwa maegesho ya magari, huku tabaka la usawa wa ardhi litatumika kwa mapokezi pamoja na huduma zingine, ghorofa la kwanza hadi la nane kutakua na ofisi za vitengo vya Ataba, kila ghorofa lina ukubwa wa mita za mraba (2m1250).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: