Mkuu wa maktaba bibi Asmahani Raádu amesema: “App imetengenezwa na kupangiliwa kisasa na rahisi kuitumia, mtumiaji anaweza kufungua kwa urahisi na kufaidika na huduma zinazo tolewa ikiwa ni pamoja na kufungua vitabu na kujisomea”.
Akaongeza kuwa: “App inasifa zifuatazo:
- Imesanifiwa vizuri na inavutia ni rahisi kuitumiwa na kila mtu.
- Inapicha nyingi za mnato na video za wasomaji wengi.
- Imepangiliwa vizuri katika ukurasa wake mkuu.
- Unaweza kushiriki katika shindano la marafiki wa maktaba kwa kusoma vitabu vingi zaidi.
- Inaingiza vitabu vipya kila wakati.
- Inafuatilia mashindano pamoja na huduma zinazo tolewa na maktaba.
- Ushirikiano wa wazi na mzuri”.
Akaendelea kusema: “App kwa sasa inapatikana kwenye vifaa vyenye (Android) na juhudi zinafanyika ipatikane kwenye vifaa vyenye (ios) pia”.