Maahadi ya Quráni tukufu inaendesha usomaji wa Quráni kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya usomaji wa Quráni kwa njia ya mtandao, kwa ushiriki wa mahafidh wa kitabu kitakatifu.

Mkuu wa Maahadi hiyo Shekh Jawadi Nasrawi amesema: Ratiba hii inalenga kuboresha hifdhu na usomaji, nayo ni katika harakati za Maahadi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, inafanywa kwa njia ya masafa, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya.

Akaongeza kuwa: “Usomaji unafanywa kupitia jukwaa la (googl meet), kila siku linasomwa juzuu moja, tutaendelea hivyo hadi mwisho wa mwezi, chini ya usimamizi wa wasomi walio bobea katika sekta hiyo, wanafuata mfumo maalum wa Quráni, tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa wasomaji wa Quráni na wamefurahia mfumo huu japokua sio wa kuhudhuria moja kwa moja”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni imeandaa mfumo maalum wa kusoma Quráni ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, wenye vipengele vingi, unao endana na mazingira ya afya pamoja na utekelezaji wa masharti ya idara ya afya, miongoni mwa vipengele hivyo ni hiki cha usomaji wa Quráni tukufu na mashindano ya Quráni pamoja na mchakato wa kuibua vipaji vya usomaji na kusaidia kuvilea, sambamba na kunufaika na mazingira mazuri ya kiroho yaliyopo katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: