Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza awamu ya pili ya shindano la kijana wa Alkafeel kwa njia ya mtandao, asubuhi ya leo Jumapili mwezi (5 Ramadhani 1442h) sawa na (18 Aprili 2021m).
Kiongozi wa harakati za vyuo vikuu Ustadh Muntadhir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya harakati za kijana mzalendo wa Alkafeel, ni matunda ya mafanikio ya awamu ya kwanza, inalenga kuongeza hazina ya elimu na utamaduni kwa vijana, kwa kujibu maswali ya shindano yanayo husu namna ya kunufaika na mwezi huu mtukufu”.
Akaongeza kuwa: “Unaweza kushiriki kwenye shindano kupitia link ifuatayo: (https://alkafeel.net/cont), baada ya kufungua link hiyo unatakiwa kujaza fumu ya ushiriki, kisha utajibu maswali, iwapo majibu sahihi yakiwa mengi yatapigiwa kura na kuchaguliwa majibu thelathini (30), wahusika watapewa zawadi maalum, aidha kutakiwa na zawadi ya kila mshiriki, majina ya washindi yatatangazwa siku ya sikuku ya Iddil-Fitri”.
Akamaliza kwa kusema: “Kwa maelezo zaidi au tatizo lolote unaweza kuwasiliana nasi kwa link maalum ya mradi wa kijana wa Alkafeel ifuatayo: https://www.facebook.com/AlKafeel.Youths/”.