Mwezi sita Ramadhani ilitolewa ahadi ya uongozi kwa Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi sita Ramadhani mwaka wa (201h) tunakumbuka moja ya matukio muhimu katika historia ya Imamu Ridhwa (a.s), nalo ni tukio la tangazo la kiapo cha ahadi ya utii kwa Imamu (a.s) kilicha tangazwa na Ma-Amuun Abbasiy pamoja na kuwa hakupenda jambo hilo.

Historia inaonyesha kuwa wito wa Ma-Amuun kwa Imamu Ridhwa (a.s) ulikua miaka miwili baada ya kuchukua utawala, alimwita na kumlazimisha akubali ahadi ya uongozi, Imamu hakuonyesha kukubali, baada ya vitisho vingi akaamua kukubali, na waliendelea kujadiliana kuhusu swala hilo kwa miezi miwili takriban.

Ma-Amuun aliendelea kusisitiza Imamu (a.s) akubali ahadi ya uongozi kwa sababu nyingi, miongoni mwa sababu zake ni kutuliza hali ya kisiasa na kutafuta uhalali wa serikali yake, na kujaribu kumbana Imamu Ridhwa (a.s) na kumuweka mbali na mji wa Madina na Iraq, na kudhofisha upinzani hususan harakati za mashia.

Imamu (a.s) alikubali ahadi ya uongozi kwa masharti, baada ya Ma-Amuun kumtishia kumuuwa, miongoni mwa masharti hayo ni; hatotoa amri, katazo, hukumu wala kubadilisha jambo lolote.

Hakika Imamu Ridhwa (a.s) hadi anafikia kuuwawa kwa sumu hakujihusisha na mambo ya serikali ispokua kwa kiwango kidogo sana kilichokua na utumishi kwa umma.

Khalifa Ma-Amuun akamwita Imamu Ali Ridhwa (a.s), na kumtaka kuondoka Madina, Imamu (a.s) akakubali kwa shingo upande, akaondoka katika mji wa Madina kwenda Khurasani makao makuu ya utawala wa Ma-Amuun. Ma-Amuun akatumia hila hiyo kujiimarisha kisiasa, akatangaza kukubali kwa Imamu ahadi ya uongozi na kushiriki katika serikali yake, ili aweze kukusanya wapinzani wake na kuunganisha nguvu za Alawiyya na Abbasiyya katika himaya yake.

Katika siku kama ya leo Ma-Amuun alifanya kikao kikubwa, akaamuru viwekwe viti viwili vya kifalme, akakaa yeye na kingine akakaa Imamu Ridhwa (a.s), halafu akamuamuru mwanae Abbasi awe wa kwanza kula kiapo cha utii, kisha akaamuru watu wote wale kiapo cha utii kwa Imamu, halafu akatoa zawadi za thamani, midani ya dhahabu ikagawiwa kwa walio hudhuria, washairi na wahadhiri wakaimba kaswida na kuongea, Ma-Amuun akaamuru Imamu atajwe kwenye mimbari zote za waislamu na pesa ziandikwe jina lake, katika mwaka huo Imamu Ridhwa (a.s) alitajwa kwenye mimbari ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (a.s.w.w) katika mji wa Madina na kuombewa dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: