Uratibu wa zaidi ya vikao (27) vya usomaji wa Quráni katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi la wilaya ya Hindiyya imeratibu zaidi ya vikao (27) vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani, vinafanywa kwenye misikiti na Husseiniyya mbalimbali kwa ushiriki wa jopo la wasomaji wa tawi.

Kiongozi wa tawi la Maahadi katika wilaya hiyo Sayyid Haamid Marábi amesema kuwa: “Hakika usomaji wa Quráni ni moja ya harakati zinazo faywa na tawi la Maahadi chini ya ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhudhuriwa na wasomi wa Quráni pamoja na waumini, chini ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza: “Usomaji unafanywa chini ya tahadhari za kujikinga na maambukizi, kama inavyo elekezwa na wizara ya afya, pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji, vikao vya usomaji wa Quráni vinafanywa ndani ya misikiti na Husseiniyya mbalimbali kwa nyakati tofauti, aidha kuna usomaji wa tartiil na usomaji wa tajwidi, wanashiriki watu wa umri tofauti”.

Kumbuka kuwa usomaji wa Quráni ni sehemu ya ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani iliyo andaliwa na Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu kwa kusoma Quráni, matawi ya Maahadi yameratibu vikao vya usomaji wa Quráni kulingana na mazingira ya kila sehemu, likiwemo tawi la wilaya ya Hindiyya katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: