Idara ya wahadhiri imeratibu majlisi za utoaji wa mawaidha katika mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa vikao vya utoaji wa mawaidha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, chini ya mradi wa tablighi uitwao Fatuma Zaharaa (a.s).

Vikao hivyo vinafanywa katika Mazaru na Husseiniyya kwenye mikoa tofauti, chini ya kufuata taratibu zote za kujikinga na maambukizi na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na uhadhiri wa makhatibu wazowefu.

Kiongozi wa idara Shekh Abduswahibu Twaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu mwezi wa Ramadhani ulipo ingia idara yetu ilianza utekelezaji wa ratiba maalum ya mwezi huu mtukufu, tunatoa mawaidha kwa utaratibu maalum, na ratiba hii itaendelea hadi mwisho wa mwezi, tunajumla ya sehemu (12) tunazo toa mawaidha chini ya taratibu zote za kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Mawaidha yanahusu utukufu wa mwezi wa Ramadhani na mafunzo ya maadili na maelekezo ya kisheria pamoja na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), pia kuna mada zinazo husu imani na athari yake kwa mtu na jamii, na namna ya kunufaika na mwezi wa Ramadhani katika kubadilisha tabia na kuachana na mambo mabaya, pamoja na kurekebisha jamii kwa ujumla, na kufanya maghafira katika mwezi huu mtukufu mwezi wa rehema”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya hufanya harakati mbalimbali ndani ya kipindi cha mwaka mzima, na katika misimu maalum huwa na harakati nyingi zaidi, ukiwemo msimu huu wa mwezi wa Ramadhani, kwani ni moja kati ya misimu muhimu kiibada, miongoni mwa majukumu yake ni kutoa mawaidha chini ya mradi wa bibi Fatuma Zaharaa na bibi Ummul-Banina (a.s) wa tablighi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: