Opresheni ya kutengeneza magari ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Idara ya mitambo chini ya kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza kazi ya kutengeneza gari za (usafi, usambazaji wa maji safi, utoaji wa maji taka, wagongwa na magari wa kubeba barafu), kwa ajili ya maandalizi maalum ya mwezi wa Ramadhani.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Alaa Abbasi Razuqi amesema: “Mafundi wa kitengo chetu hufanya matengenezo ya gari zilizo chini yao kila wakati, lakini kuna matengenezo makubwa ambayo hufanywa baada ya kumaliza msimu wa ziara au tunapo karibia msimu wa ziara ili kuziweka tayali kwa ajili ya kutekeleza majukumu”.

Akasema: “Matengenezo hayo yanafanywa kwa kufuata ratiba maalum bila kuathiri shughuli zingine, gari zote zinakaguliwa kila sehemu, hasa gari za kufanya usafi na kubeba taka ambazo hufanya kazi wakati wote, pamoja na gari za kubeba barafu (RO) na gari za kusambaza maji safi ya kunywa”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili kinamiliki gari nyingi za kimkakati, zinazo toa huduma tofauti kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: