Vikao vya usomaji wa Quráni katika mkoa wa Najafu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imeratibu zaidi ya vikao tisa vya usomaji wa Quráni katika mkoa wa Najafu kupitia tawi la Maahadi, katika maeneo tofauti ndani ya mkoa, visomo vitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu, chini ya tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.

Kiongozi wa tawi la Maahadi Sayyid Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika usomaji wa Quráni unafadhila nyingi katika kila siku ndani ya mwaka, na katika mwezi wa Ramadhani fadhila zake na thawabu huwa nyingi zaidi, ukisoma aya moja ndani ya mwezi wa Ramadhani unaandikiwa thawabu sawa na aliyesoma Quráni nzima katika miezi ya kawaida, kutokana na utukufu huo ndipo Maahadi na matawi yake yakaandaa ratiba za usomaji wa Quráni tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Maandalizi ya usomaji wa Quráni yalianza mapema, ziliandaliwa sehemu za kusomea na kubaini idadi ya wasomaji, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ratiba inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa”.

Kumbuka kuwa matawi ya Quráni tukufu katika mji wa Karbala na mikoani, yanatekeleza ratiba zao maalum za mwezi huu mtukufu, ikiwemo ratiba ya usomaji wa Quráni tukufu inayo endeshwa katika Husseiniyya na mazaru tofauti kwa kuzingatia kanuni za kujikinga na maambukizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: