Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi za mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya, inafanya majlisi za mwezi wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa Aljuud pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, zitaendelea hadi mwisho wa mwezi, kwani zipo ndani ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya katika mwezi huu mtukufu, sambamba na kuhakikisha muda unatumiwa vizuri.

Kiongozi wa idara hiyo, mhadhiri wa majlisi Shekh Swahibu Twaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunafanya majlisi kwa kufuata maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na hufanywa kila siku jioni baada ya swala ya Magharibaini, imeteuliwa sehemu maalum ya kufanyia majlisi hizo, baada ya kuwa hapo awali zilikua zinafanywa ndani ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mwaka huu kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, imeandaliwa sehemu maalum katika ukumbi wa Aljuud na kuweka vifaa vyote vya kujikinga na maambukizi, ikiwa ni pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji”.

Akaongeza kuwa: “Vikao hivi vinafanywa chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), unaolenga kuhuisha matukio ya kidini, mwezi mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa misimu muhimu ya kiibada, ambao lazima tunufaike nao, ni mwezi ambao siku zake ni bora kushinda siku zingine zote, ni mwezi ambao tumeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu”.

Akasema kuwa: “Mada tofauti zinazungumzwa katika majlisi hizo, tunazingatia pia kuadhimisha matukio yaliyopo ndani ya mwezi huu, kama vile kifo cha bibi Khadija na kuzaliwa kwa Imamu Hassan pamoja na kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) na matukio mengine, vilevile huzungumzwa mambo ya kifiqhi, kiaqida, kimaadili, na mambo mengine kulingana na utukufu wa mwezi huu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya mwezi huu mtukufu, inayo husisha majlisi zinazo fanywa kwa njia ya mtandao na zinazo hudhuriwa moja kwa moja kwa kufuata kanuni za kujikinga na maambukizi, ikiwemo majlisi hizi ambazo hufanywa kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: