Maahadi ya Quráni tukufu: Bagdad yasimamia vikao (30) vya usomaji wa Quráni katika mji wa Karkha na Raswafa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya itengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia tawi la Maahadi katika mji mkuu wa Bagdad, imeratibu vikao (30) vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani vinavyo fanywa ndani ya misikiti na Husseiniyya za mji wa Karkha na Raswafa.

Mkuu wa Maahadi hiyo Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma Quráni kwa mazingatio, na kumuweka mwanaadamu katika uongofu na nuru, na kufanyia kazi kauli ya Imamu Baaqir (a.s): isemayo (Kila kitu kinamsimu na msimu wa Quráni ni mwezi wa Ramadhani), tawi la Maahadi katika mkoa wa Bagdad limeandaa vikao (30) vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi huu mtukufu, wameshiriki wasomi wa Quráni tukufu na wamechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ikiwa ni pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu”.

Akaongeza kuwa: “Visomo vinafanywa kwa kufuata ratiba maalum ili kutoa nafasi kwa washiriki wengi zaidi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuna mwitikio mkubwa sambamba na mazingatio mazuri ya kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine, linatekeleza ratiba maalum ya usomaji wa Quráni katika mwezi wa Ramadhani ndani ya Misikiti Husseiniyya na Mazaru takatifu na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: