Mwaka umepita tangu kukamilika kwa jengo ya Alhayaat katika mji wa Najafu

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku kama ya leo tarehe (22 Aprili 2020m), kilikamilisha ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa mtukufu wa Najafu, kwenye eneo la hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s), siku hizo kulikua na ongezeko ya maambukizi, jambo lililo pelekea kujengwa vituo vya Alhayaat kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.

Ujenzi wa vituo vivyo ulitokana na kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia taasisi za afya, na chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ujenzi huo ulilenga kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa na kutoa huduma bora za matibabu.

Jengo hilo lilikamilka wiki moja kabla ya muda uliotarajiwa, lilijengwa kwa muda wa siku kumi na nane tu, na lilitarajiwa kujengwa kwa muda wa siku (25), ni jengo ambalo limekamilisha vigezo vyote vya kiufundi na kitaalamu, kulingana na matumizi yake, linaukubwa wa mita za mraba (600), linavyumba vya wagonjwa (24) na vyumba maalum vya wauguzi na madaktari, jengo linamahitaji yote muhimu (umeme, viyoyozi, vimamoto, oksijen na mengineyo).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia watumishi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi imekua ikijenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe (25 Machi) hadi (25 Aprili) imefanikiwa kujenga vituo vitatu, navyo ni jengo la Alhayaat la pili katika hospitali ya Hussein (a.s), na jengo la Alhayaat la tatu katika hospitali kuu ya Hindiyya mkoani Karbala, pamoja na jengo hili katika mji wa Najafu, yakafuata majengo mengine yaliyo jengwa haraka pamoja na changamoto za wakati huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: