Mahafali za usomaji wa Quráni za wanawake zinaratibiwa na Maahadi ya Quráni tawi la wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa mahafali za usomaji wa Quráni tukufu kwa wanawake, katika makao makuu ya tawi mjini Najafu na kwenye matawi yake ya mikoani, chini ya ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, iliyo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu, na itaendelea hadi mwisho wa mwezi, na kuhakikisha tunanufaika na usomaji wa Quráni tukufu kwa kufanya vikao hivi vinavyo hudhuriwa na malaika mwengi wa rehema.

Kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tulianza kufanya vikao vya usomaji wa Quráni tukufu tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani, tunatumia njia mbili katika kufanikisha jambo hili kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi kwa Korana, njia ya kwanza ni wasomaji kuhudhuria moja kwa moja katika vikao vya usomaji wa Quráni, na kufuata masharti yote ya kujikinga na maambukizi ikiwa ni pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, njia ya pili ni masafa, kwa kutumia mtandao kupitia link ifuatayo https://meet.google.com/hen-fris-tao”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake kila mwaka ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani huwa na ratiba maalum, yenye vipengele tofauti katika siku zote za mwezi mtukufu, kutokana na mazingira ya mwaka huu pamoja na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, aliye husia kujiepusha na mikusanyiko, tumeamua kutumia njia hizi kufikisha sauti ya wanawake na kuhakikisha harakati hazisimami.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: