Mawakibu Husseiniyya zimeanza opresheni ya kugawa chakula cha mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetangaza kuwa, wawakilishi wake na idara zanazo fungamana nao pamoja na mawakibu za kutoa huduma, zimeanza opresheni kubwa ya kugawa chakula cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, ili kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika mazingira haya magumu kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, na kupanda bei ya vyakula.

Miongoni mwa idara zilizo anza kutoa misaada ni idara za mawakibu za wilaya ya Madaaini katika mkoa wa Bagdad, kiongozi wa idara hiyo bwana Hussein Hassan Mahusi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kipindi chote cha mwaka huwa tunatoa misaada, lakini mwezi wa Ramadhani huwa kuna misaada maalum, huwa tunaongeza kiwango cha utoaji wa misaada kwa ajili ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, kabla ya kuingia mwezi mtukufu tuliandaa utaratibu ulioshirikisha mawakibu zote, na kuhakikisha tunagawa chakula kwenye kila kitongoji, tutaendelea kugawa hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu”.

Akaongeza kuwa: “Katika siku ya kwanza tuligawa vifurushi vya chakula (165) kwa familia zinazo ishi katika kitongoji cha Jisru, Zaáfaraniyya na maeneo mengine, kisha tukaenda katika vitongoji vingine na tunaendelea kugawa misaada kila siku”.

Kumbuka kuwa rais wa kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhu Niímah Salmaan, alisema kuwa: “Toka ulipo ingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma zilizo chini ya kitengo hiki kwenye mikoa tofauti, zimekua zikigawa chakula kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, chini ya utaratibu maalum na tunatarajia kusaidia famila nyingi iwezekanavyo katika kila eneo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: