Mwezi kumi Ramadhani kumbukumbu ya kifo cha mama wa waumini bibi Khadijatul-Kubra (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi wa Ramadhani unamatukio mengi ya kihistoria, yapo ya furaha na huzuni, miongoni mwa matukio ya huzuni kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), ni kifo cha mama wa waumini mke wake kipenzi bibi Khadijatul-Kubra (a.s) aliye kufa tarehe kama ya leo mwezi kumi Ramadhani.

Naye ni mke wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w), hakuowa mwanamke mwingine katika maisha yake matukufu kwa ajili ya kumtukuza na kumuheshimu, alikuwa wa kwanza kuingia katika uislamu na alijitolea mali yake kwa ajili ya uislamu, yatosha fahari kwake kuwa mama wa Swidiqatu-Zaharaa (a.s) ambaye Mwenyezi Mungu amejalia familia ya Mtume (s.a.w.w) kuendelezwa na yeye.

Bibi Khadija (a.s) ndio mwanamke wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w) na akamsadikisha, akaswali naye swala ya kwanza na kutangaza uislamu wake, ni mwanamke wa kwanza kumlinda Mtume (s.a.w.w) na kujitolea mali zake zote, ni mwanamke wa kwanza ambaye Imani yake ilikamilika kwa kumtawalisha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema: (Dini haikusimama ispokua kwa vitu viwili: mali ya Khadija na upanga wa Ali bun Abu Twalib (a.s)), na anasema: (Sijawahi kunufaishwa na mali kama ilivyo ninufaifa mali ya Khadija (a.s)).

Hakika alikua na hadhi kubwa sana, hadi Mtume (s.a.w.w) akasema: (Wabora katika wanawake wa ulimwenguni ni wane: Maryam bint Imaran, Asia mwanamke wa Firáun, Khadija bint Khuwailid na Fatuma bint Muhammad).

Baada ya miaka kumi ya utume na miaka mitatu kabla ya kuhama, mama hiyu mtakatifu alifariki dunia na kuacha jeraha na maumivu makubwa katika moyo wa Mtume (s.a.w.w) na umma wa kiislamu kwa ujumla, alikua bibi mtakatifu na nguzo muhimu kwa Mtume (s.a.w.w), jambo lililo ongeza huzuni kwa Mtume (s.a.w.w) alikufa mwaka aliokufa Ammi yake Abu Twalib (r.a), aliyekua nguzo yake muhimu kwenye upande wa siasa na jamii, hakika Mtume hakuusahau mwaka huo maisha yake yote, na akauita (mwaka wa huzuni).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: