Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi kumi Ramadhani, ni siku ya kumbukumbu inayo huzunisha sana iliyo muumiza Mtume Muhammad (s.a.w.w), kumbukumbu ya kifo cha mama wa waumini mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Khadijatul-Kubra (a.s), kifo chake kiliacha maumivu na huzuni kubwa katika moyo wa Mtume (s.a.w.w) na umma wa kiislamu kwa ujumla.

Kutokana na kuomboleza tukio hilo na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kwa msiba huu, Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi, yanayo ashiria huzuni na majonzi, yamewekwa mabango yenye jumbe tofauti za maombolezo.

Aidha imeandaliwa ratiba maalum ya kuomboleza inayo endana na hali ya mazingira ya sasa kiafya, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeweka utaratibu maalum wa kupokea mawakibu za waombolezaji zitakazo kuja katika malalo hii takatifu.

Kumbuka kuwa mama wa waumini bibi Khadijatul-Kubra (a.s) Mwenyezi Mungu amempa utukufu maalum, ambao hajampa mwanamke yeyote duniani, alikuwa mtu wa kwanza kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake mtukufu (s.a.w.w) katika wanawake, akavumilia matatizo mengi pamoja na Mtume (s.a.w.w), alijitolea mali zake zote kwa ajili ya uislamu, bali alijitolea hadi nafsi yake kwa ajili ya mbora wa walimwengu na bwana wa Manabii na Mitume, kwa ajili ya kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: