Wito wa kushiriki katika ratiba ya (Familia na tunda ya Quráni)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa wito kwa watoto wa kike wajitokezo kushiriki katika program ya (Familia na tunda la Qur’ani itakayo fanywa kwa njia ya mtandao).

Kiongozi wa kituo hiki bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: Kuna program ya kimalezi na kimaadili itakayo endeshwa na kituo chetu katika mwezi huu mtukufu, kwa kuwa huu ni mwezi wa Qur’ani, tumetumia aya za Qur’ani tukufu kufanikisha tunacho kusudia, na namna ya kunufaika na aya hizo katika familia chini ya mwenendo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Akaongeza kuwa: Asilimia kubwa ya aya za Qur’ani tukufu ni muongozo na taa la misingi ya familia, zinaweza kufanyiwa kazi katika maisha ya familia ambayo mwanamke ndio msingi wa maisha hayo, tumeunda kamati ya wataalamu itakayo simamia program hiyo itakayo endeshwa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: