Waziri wa Utamaduni na wakazi wamesema: Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya kazi kubwa tunayo jivunia wote

Maoni katika picha
Waziri wa utamaduni na utalii Dokta Hassan Naadhim na waziri wa kazi na mambo ya kijamii Dokta Aadil Rikabi, wamesema kuwa uwezo walio uona katika chuo kikuu cha Alkafeel ni sawa na vyuo vya nchi zilizo endelea, jambo hili ni fahari kwezu wote.

Wamesema hayo siku ya Alkhamisi Ramadhani tisa (1442h) sawa na tarehe (22 Aprili 2021m) wakiwa pamoja na rais wa chuo cha Bagdad na chuo cha Kufa, walipo tembelea chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupokewa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na rais wa chuo Dokta Nuris Shahidi Dahani wakiwa pamoja na rais wa chuo cha Al-Ameed na rais wa kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Dokta Aadil Rikabi amesema: “Leo tumetembelea chuo kikuu cha Alkafeel, kwa hakika tumefurahishwa sana na tulicho kiona na kusikia, majengo ni mazuri yana vivaa bora vya kisasa na walimu mahiri wenye uwezo mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Tutapeleka uzowefu huu kwenye vituo vingine vya elimu mjini Bagdad na kwenye mikoa mingine, watu wengi hawakijui chuo hiki wala hawajui uwezo wake, kwa hakika tunakitakia mafanikio mema, na tunamshukuru rais wa chuo kwa kutuonyesha mambo yaliyopo katika chuo hiki na kazi kubwa wanayo fanya, aidha tunawaomba wanafunzi wasipoteze fursa adhim ya kunufaika na chuo huki”.

Mawaziri hao wametembelea maeneo mbalimbali ya chuo, wakiwa pamoja na rais wa chuo, aliye eleza mazingira ya chuo pamoja na mikakati ya baadae, ikumbukwe kuwa chuo hiki kimejengwa chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kuongeza kiwango cha elimu hapa Iraq.

Tambua kuwa chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kila kiwezalo kuboresha uwezo wake katika sekta ya elimu na utamaduni pamoja na tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: