Maahadi ya Quráni inafanya mashindano ya mwezi wa Ramadhani yaliyopewa jina la (maneno ya nuru)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya mashindano ya Quráni kwa njia ya redio yaliyo pewa jina la (maneno ya nuru) kwa kushirikiana na idhaa ya Babelon katika usomaji, hukumu na tafsiri.

Shindano linarushwa mubashara kila siku ya Jumamosi saa kumi na nusu Alasiri, chini ya usimamizi wa kiongozi wa usomaji katika tawi la Maahadi Ustadh Luay Watwifi, pamoja na kamati ya majaji, hukumu za usomaji zinasimamiwa na kiongozi wa tawi Sayyid Muntadhiri Mashaikhi, na hukumu za kusimama na kuanza Ustadhi Nabiil Asadi, na tafsiri Shekh Hassan Maámuri.

Kumbuka kuwa shindano linahusisha kila mtu, kila kipindi hupatikana mshindi na kupewa zawadi, naye ni yule atakaepata alama nyingi zaidi katika usomaji, na katika tafsiri ikitokea kugongana majibu sahihi, hupigwa kura ili kumpata mshindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: