Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha umeme katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kusaidia miradi ya kitaifa inayo lenga kuhudumia wananchi wa Iraq, chini ya wizara mbalimbali, hivi karibuni imetoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha umeme kaskazini ya Karbala.

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Muhandi Yusufu amesema: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu iko mstari wa mbele katika kusaidia miradi ya umeme hapa mkoani, siku za nyuma ilitoa kiwanja kwa ajili ya kujenga kituo cha umeme katika kitongoji cha Ibrahimiyya, na leo imetoa kiwanja kingine kwa ajili ya kujenga kituo cha umeme”.

Akaongeza kuwa: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kituo hiki kinatarajiwa kuzalisha kilowat (133) zitakazo saidia kuziba pengo lililopo katika kituo kikuu cha umeme hapa mkoani, aidha kitasaidia kuanzishwa kituo kingine cha pili”.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ilisaidia ujenzi wa kituo cha umeme Alkafeel mwaka jana, ili kupunguza mzigo kwenye kituo kikuu cha umeme katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: