Ataba mbili tukufu zinatoa pole kwa wahanga wa tukio la hospitali ya ibun Khatwibu

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinatoa pole kwa wahanga wa moto ulio tokea katika hospitali ya ibun Khatwibu katika mji mkuu wa Bagdad, ulio sababisha vivyo vya baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa pamoja na majeruhi.

Pole imetolewa kupitia ujumbe wa Ataba mbili tukufu uliokuja leo asubuhi ya mwezi (13 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (26 April 2021m) uliokuja kukutana na wahanga wa janga hilo na kuwapa pole, ujumbe huo umehusisha baadhi ya viongozi wa Ataba mbili tukufu na watumishi wao, umefikisha pole kutoka kwa Marjaa Dini mkuu na viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba hizo pamoja na watumishi wa malalo mbili takatifu kwa familia za wafiwa na majeruhi.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika ugeni huo ambaye ni makamo rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakili amesema: “Kwa mujibu wa maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili takatifu tumekuja kushiriki katika vikao vya kuomboleza watu waliokufa katika tukio la moto uliotokea kwenye hospitali ya ibun Khatwibu, na kuwapa pole wafiwa pamoja na kuwahakikishia kuwa tupo pamoja nao katika wakati huu mgumu, tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa mwezi huu awarehemu maiti wetu na kuwapa subira na uvumilivu wafiwa”.

Akafafanua kuwa: “Katika siku ya kwanza ya ziara yetu tutashiriki katika vikao vya uombolezaji wa marehemu wote, tumeanza kukaa kwenye vikao hivyo tangu asubuhi na bado tunaendelea hadi muda huu, kesho tutatembelea watu walio jeruhiwa katika tukio hilo”.

Wafiwa wameshukuru sana ujio wetu, jambo hili sio geni kufanywa na Ataba mbili tukufu, kwa aina ya pekee wamepongeza ujio wetu na kushiriki katika shughuli za uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: