Kuanza usajili wa shindano la kuhifadhi Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi lake la mkoa wa Najafu, imeanza kusajili washiriki wa shindano la kuhifadhi Quráni la mwaka wa tatu, ndani ya mwezi wa Quráni mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kujenga moyo wa kushindana katika jambo tukufu zaidi la Quráni takatifu.

Shindano hili linafanywa kwa mwaka wa tatu mfululizo, linalenga kuadhimisha kitabu cha Mwenyezi Mungu katika nafsi za washiriki, na kunufaika na mwezi huu mtukufu kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu pamoja kushajihisha kuhifadhi na kusoma kwa ufasaha kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Masharti ya shindano:

  • - Mshiriki achague moja ya vikundi vitatu cha shindano (juzuu 5, juzuu 10, juzuu 20).
  • - Shindano ni kwa wanaupe tu.
  • - Shindani ni maalum kwa wakazi wa mkoa wa Najafu.
  • - Haifai mshiriki kuchagua chini ya kiwango cha juzuu kilicho tajwa.
  • - Siku ya mwisho ya usajili ni Jumanne ya mwezi (21 Ramadhani).
  • - Usajili unafanywa kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/onKS3M1bhvf1Upkb6.

Maahadi imeandaa zawadi za washindi watatu wa mwanzo katika kila kikundi, kwa maelezo zaidi piga simu (07601663569).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: