Mwezi 15 Ramadhani imeangaza nuru ya Mwenyezi Mungu katika ardhi kwa kuzaliwa Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Ardhi imeangaza nuru ya Mwenyezi Mungu kwa kuzaliwa mjukuu wa Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s), katika siku kama ya leo mwezi kumi na tano Ramadhani mwaka wa tatu hijiriyya, nyumba ya Mtume katika mji wa Madina ilitangaza kuzaliwa kwa mjukuu wa kwanza wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), baada ya Mtume kupewa habari akaenda katika nyumba ya Zaharaa (a.s) kumuangalia mtoto aliye zaliwa.

Kutoka kwa Imamu Ali bun Hussein (a.s) anasema: (Fatuma alipo mzaa Hassan (a.s) alimuambua Ali (a.s) mpe jina. Akasema: siwezi kumtangulia Mtume wa Mwenyezi Mungu, mara Mtume (s.a.w.w) akaja, akapewa mtoto akiwa amefunikwa kitambaa cha njano, akasema: sijakukatazeni kumfunika mtoto na kitambaa cha njano? Akamfunua, kisha akamfunika kitambaa cheupe, halafu akamuuliza Ali (a.s): umempa jina? Akasema: siwezi kukutangulia kumpa jina. Akasema (s.a.w.w): na mimi siwezi kumtangulia Mwenyezi Mungu mtukufu katika kumpa jina.

Mwenyezi Mungu akamuambia Jibrilu kuwa, katika nyumba ya Muhammad amezaliwa mtoto, nenda ukampe salamu na pongezi, umuambie: hakika Ali kwako ni sawa na Haruna kwa Mussa, mpe jina la mtoto wa Haruna. Jibrilu (a.s) akaenda na kumpa salam na pongezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu anakuamuru umpe jina la mtoto wa Haruna. Akasema jina lake alikua nani? Akasema: Shabiri. Kwa kiarabu mwite Hassan, ndipo akaitwa Hassan. Alizaliwa (a.s) katika mji wa Madina usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani mwaka wa tatu hijiriyya.

Akakua chini ya malezi ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akajifunza tabia njema kutoka kwa babu yake, aliendelea kuwa karibu naye hadi alipo fariki dunia, alimrithisha uongofu wake, haiba, unyenyekevu na akamuandaa kwa Uimamu uliokua unamsubiri baada ya baba yake kiongozi wa waumini, babu yake alikuwa amesha sema swala hilo katika matukio tofauti, miongoni mwa matukio hayo ni pale aliposema: (Hassan na Hussein ni maimamu wakiwa wamesimama au wamekaa, ewe Mwenyezi Mungu mimi nawapenda nawe mpende atakae wapenda).

Hakika alikua na utukufu wa Utume na Uimamu, pamoja na utukufu wa hadhi na nasabu, waislamu walipata kwake yale waliyopata kwa babu yake na baba yake, hadi walikua kila wanapo muangalia wanawakumbuka (baba na bubu yake), wakampenda na kumtukuza, alikua kimbilio lao wa pekee baada ya baba yake, walimfuata kwa kila tatizo la Dini na dunia, hususan baada ya umma wa kiislamu kuingia katika wakati mgumu usiokua na mfano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: