Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimemaliza mashindano ya Quráni katika mji wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Wawakilishi wa Mawakibu za Diwaniyya chini ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wamemaliza mashindano ya Quráni awamu ya tano katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, yaliyo anza kwabla ya siku kumi, na kushiriki idadi kubwa ya mawakibu Husseiniyya za mji huo.

Jioni ya Jumanne mwezi (14 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (27 Aprili 2021m), sambamba na kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s), mashindano ya Quráni tukufu yamekhitimishwa mbele ya ujumbe uliowakilisha wageni waalikwa.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Hii ni moja ya harakati zinazo fanywa na kitengo chetu, mwaka huu tumefanya kwa mara ya tano ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, washiriki huwa ni vikundi vya wasomaji wa Quráni, huulizwa maswali ya usomaji, tafsiri na hifdhu”.

Akaongeza kuwa: “Shindano linalenga kujenga moyo wa kujifunza Quráni na limefanyika kwa muda wa siku kumi chini ya jopo maaluma la majaji, kikundi cha Hassan Almujtaba (a.s) kimepata nafasi ya kwanza, na kikundi cha watumishi wa Fatuma Zaharaa (a.s) nafasi ya pili, na kikundi cha njia ya mapambano ya Hussein (a.s) nafasi ya tatu, wote wamepewa zawadi kutoka katika kitengo chetu”.

Kumbuka kuwa mawakibu Husseiniyya hakiishii kutoa huduma kwa mazuwaru wakati wa ziara peke yake, bali zinaharakati mbalimbali za kielimu na kitamaduni, pamoja na huduma tofauti za kibinaadamu zinazo kamilisha jukumu lake la msingi la kuhudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: