Kituo cha utamaduni wa familia chino ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya shindano la wanawake kwa njia ya mtandao liitwalo (Mjukuu wa Mtume), linahusu historia ya Imamu Hassan (a.s).
Mkuu wa kituo hicho, bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili ni moja ya mashindano yanayo simamiwa na kituo, katika kuadhimisha mazazi ya Maimamu watakatifu (a.s), likiwemo tukio hili la mwezi kumi na tano Ramadhani, linalo lenga kuangazia historia takatifu ya Imamu Hassan (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Shindano hili ni kujibu maswali yanayo muhusu Imamu anaye adhimishwa, maswali yanayo sababisha mshiriki asome vitabu vya historia ilia kupata majibu sahihi”.
Akabainisha kuwa: “Shindano linafanyika kupitia mtandao, na litadumu kwa muda wa siku tatu kuanzia leo, kuna zawadi za washindi watatu wa mwanzo”.