Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inafanya shindano la (Rabiul-Quluub)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, linaendesha shindano la (Rabiul-Quluub) la Quráni ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amesema: “Hili ni shindano maalum kwa wanafunzi wa Maahadi, linasehemu tofauti, (kuhifadhi juzuu tatu, kuhifadhi juzuu tano, na kuhifadhi juzuu kumi), kila kundi la sehemu hizo limegawanyika sehemu tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Shindano hili linalenga kujenga moyo wa usomaji wa Quráni kwa wanafunzi, na kuendelea kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akasema: “Shindano linafanywa kupitia program ya (Google meet) chini ya kamati ya majaji walio bobea, majina ya washindi wa kila kikundi yatatangazwa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake inalenga kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, ikiwemo elimu ya (maarifa ya Quráni) pamoja na kujenga jamii ya wanawake wajuzi wa Quráni wenye uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali katika somo la Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: