Kitu gani kinachofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Sanjaar ndani ya mwezi mtukufu?

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani katika wilaya ya Sanjaar kaskazini magharibi ya mkoa wa Mosul, kupitia kituo chake cha maelekezo na utamaduni katika mwezi wa rehema, na maghafira, mwezi wa Ramadhani pamoja na ujumbe wake wa kidini na kimaadili.

Msimamizi wa program hii Shekh Haidari Aáridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika program hii inafanywa kwa mwaka wa nne mfululizo, na inavipengele vingi kikiwemo cha vikao vya usomaji wa Quráni na vikao vya mawaidha yenye mafundisho mbalimbali ya kidini, harakati zote hufanywa ndani ya ukumbi wa kituo na kuhudhuriwa na wakazi wa mji huo kwa kufuata masharti ya kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa kituo hakilengi kundi maalum, bali kinatoa huduma kwa makundi yote ya Sunni, Shia, Turkuman, Aizidiyyin na Wakurdi, huwa na vipengele vingi vinavyo lenga kuhudumia wakazi wa Sanjaar kwa ujumla, baada ya matatizo waliyopata katika kipindi walicho tekwa na magaidi wa Daesh, hivyo tunajitahidi kutoa malezi ya kidini, kimaadili na kifikra kwa kizazi kijacho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: