Mwezi kumi na saba ramadhani ilipiganwa vita ya Badri

Maoni katika picha
Siku ya Ijumaa imesadifu kumbukumbu ya vita ya Badri iliyo tokea mwezi (17) Ramadhani mwaka wa pili Hijiriyya, nayo ni vita ya kwanza kijeshi kati ya waislamu na makafiri wa kikuraishi, pia ndio vita mashuhuri iliyo ongozwa na Mtume (s.a.w.w) dhidi ya makafiri, mshika bendera alikua ni Ali (a.s) akiwa na umri wa miaka (25).

Imepewa jina hilo kutokana na jina la sehemu ilipo fanyika, sehemu yenye kisima cha Badri katikati ya Maka na Madina, pia palikua na soko la waarabu na moja ya sehemu za kukutana kwao na kubadilishana biashara, waarabu walikua wanakutana hapo kila mwaka.

Sababu za vita hiyo Wakuraishi walikuwa wanawanyanyasa Waislamu, hadi Waislamu wakaamua kuhama Maka na kwenda Madina, baada ya Waislamu kukimbia Maka Makuraishi wakapora mali za waislamu na wakaendelea kuwanyanyasa.

Vita ya Waislamu na Makafiri ilianza baada ya Makafiri kuvamia maeneo ya waislamu, na iliendelea hadi waislamu walipo pata ushindi, kisha Mtume akaamuru kuzikwa maiti za waislamu na kufukiwa maiti za maadui, kisha akawasalisha waislamu swala ya Alasiri na wakaondoka kwenda Madina wakiwa na furaha ya ushindi waliopata.

Ushindi huo ukaimarisha ngome ya waislamu, habari zikaenea katika eneo lote la uarabuni, kila mtu akaanza kuuogopa usialamu.

Ikaandikwa historia ya ushindi wa waislamu katika vita ya kwanza, ushindi ulio onesha ushujaa wa bani Hashim hususan Imamu Ali (a.s), baadhi ya vitabu vya historia vimeandika kuwa watu walio uwawa na Imamu Ali katika vita hiyo walifika (35) na baadhi ya vitabu vimeandika hadi majina yao..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: