Maahadi ya Quráni tukufu imetangaza kutolewa kwa fomu ya kujisajili katika shindano la surat Israa

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza fomu ya usajili kwa wanaopenda kushiriki kwenye shindano la kuhifadhi surat Israa.

Maahadi ya Quráni katika tangazo hilo imesema kuwa: “Fomu ya usajili wa shindano hilo itatolewa siku ya tarehe (16) Ramadhani”. Akabainisha kuwa: “Zawadi zimeandaliwa kwa washindi wa mwanzo”.

Akaongeza kuwa: “Kuna masharti mawili ya kukubaliwa kushiriki kwenye shindano hili, kwanza mshiriki awe na umri wa miaka (20) na asiwe amehifadhi Quráni nzima”.

Maahadi imepanga siku ya Alkhamisi tarehe (27) Ramadhani sawa na tarehe (10/05/2021m) itakua ndio shiku ya shindano, shindano litaanza saa mbili asubuhi mbaka saa sita mchana”.

Link ya kutumia kujaza fomu ni: https://bit.ly/3xBBt9I
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: