Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetengeneza masafa ya kurusha matangazo mubashara bure kwa vyombo vya habari katika siku za Lailatul-Qadr

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishani wa vipindi Alkafeel na matangazo mubashara chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetengeneza masafa ya kurusha matangazo bure yenye ubora mkubwa wa kiwango cha (HD) katika siku za Lailatul-Qadr.

Na kimetoa wito kwa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kuonyesha matukio ya siku hizo takatifu, watumie masafa hiyo kupitia anuani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)

‏DOWNLINK:12680.200 H

‏MOD:DVBS2

‏QPSK

‏FEC:5/6

‏Sr :3250

‏HD/MPEG-4


Tambua kuwa ratiba ya matangazo ya moja kwa moja (mubashara) itakua kama ifuatavyo:

 • - Swala ya Adhuhuri kwa mujibu wa wakati wa Karbala tukufu.
 • - Usomaji wa Quráni kuanzia saa 11:00 hadi 12:00 Jioni.
 • - Swala ya Magharibi kwa mujibu wa wakati za Karbala.
 • - Dua Iftitaah, saa 2:00 usiku.
 • - Ziara ya Imamu Hussein (a.s) katika usiku wa Lailatul-Qadri.
 • - Dua ya kubeba misahafu.
 • - Dua ya Jaushen-Kabiir, kuanzia saa 4:00 hadi saa 6:00 usiku.
 • - Mawaidha yatakayo tolewa na Shekh Abdu-Swahibu Twaaiy kuanzia saa 6:00 usiku.
 • - Dua ya Abu Hamza Shimali kuanzia saa 7:00 hadi saa 8:00 usiku.
 • - Dua za usiku, kuanzia saa 9:00 usiku na kuendelea.
 • - Swala ya Alfajri kwa mujibu wa wakati wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: