Kumbukumbu ya kuvunjika nguzo ya uongofu na kuondoka ngome

Maoni katika picha
Mwezi kumi na tisa Ramadhani, ni siku ya kumbukumbu inayo sikitisha ya kujeruhiwa kwa wasii wa Mtume na Imamu muadilifu kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), alfajiri ya siku hiyo alijeruhiwa na muovu zaidi ya waovu wa mwanzo na wamwisho ibun Muljim Almuraadi.

Alfajiri ya mwezi kumi na tisa Ramadhani mwaka wa (40h), ibun Muljim alimpiga upanga wenye sumu kali Imamu Ali (a.s) akiwa anaswali katika msikiti wa Kufa.

Riwaya zianaonyesha kuwa kiongozi wa waumini alipotaka kwenda msikitini katika siku aliyo pigwa upanga, alizungukwa na bata wakiwa wanalia na kumzuwia asitoke lakini aliwafukuza na akasema, waacheni hakika uliaji wao utafuatiwa na vilio…

Kutoka kwa Sharifu Ridhwa (r.a) anasema: Ali (a.s) katika usiku aliopigwa upanga alikuwa amekesha, akasema mimi nitauwawa kukipambazuka, palipo adhiniwa akaondoka kwenda asikitini, akatembea kidogo kisha akasimama, binti yake Zainabu akamuambia: Ewe kiongozi wa waumini muambie Juúdah aswalishe watu, akasema: hauwezi kukinbia ahadi, halafu akaenda.

Katika hadithi nyingine alisema: Alikua (a.s) anaangalia tandiko lake lakini halali, kisha anaangalia mbinguni na kusema: Wallahi sijawahi kudanganya wala kudanganywa, hakika huu ndio usiku nilio ahidiwa, ilipo fika Alfajiri akafunga msuli wake huku anasema:

Funga msuli wako kwa ajili ya kifo hakika kifo kitakukuta

Wala usiogope kifo unapofika wakati wake.

Imamu (a.s) akatoka kwenda kuswalisha watu, aliposujudi katika mihrabu yake ndipo mal-uuni ibun Muljim akampiga kwa upanga wenye sumu kali kichwani kwake, Imamu (a.s) akasema: nimefauli kwa haki ya Mola wa Alkaaba.

Ndio. Hakika Imamu Ali (a.s) alifaulu kwa kupata kifo cha kishahidi, aliuwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ndani ya msikiti wa Mwenyezi Mungu na katika mwezi wa Mwenyezi Mungu, na aliye muuwa ni kiumbe muovu zaidi wa Mwenyezi Mungu.

Watu wakamzunguka kiongozi wa waumini (a.s) akiwa katika mihrabu yake, akifunga jeraha lake na kuweka udongo sehemu alipo umia, kisha akasoma maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo: (Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tutakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyingine) kisha (a.s) akasema: Imekuja amri ya Mwenyezi Mungu na amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Riwaya zinasema kuwa malaika walilia na upepo mweusi ukavuma, milango ya msikiti ikajifunga, malaika Jibrilu akasema:

(Wallahi nguzo ya uongofu imevunjika, wallahi nyota za mbinguni zimezimika na ngome imeondoka, ameuwawa mtoto wa Ammi wa Mtume, ameuwawa wasii mteule, ameuwawa Ali mridhiwa, ameuwawa bwana wa mawasii, kauliwa na muovu zaidi ya waovu).

Watu walipo sikia kelele wakakimbilia msikitini, wakawa wanazunguka wala hawajui wafanye nini kutokana na ukubwa wa mshtuko, wakamzunguka kiongozi wa waumini (a.s) akiwa anafunga jeraha lake kwa msuli wake, huku damu inachirizika usoni kwake, ndevu zikiwa zimelowa damu, huku anasema: hiki ndio alicho ahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Kisha wakambeba kiongozi wa waumini (a.s) hadi nyumbani kwake, wakamkuta Zainabu na Ummu-Kulthumu pamoja na wanafamilia wengine wamesimama mlangoni wanamsubiri, walipo muona akiwa katika hali hiyo, wakaanza kulia na kusema: Ewe baba! Ewe Msiba…

Imamu Ali (a.s) akaugulia maumivu kwa muda wa siku tatu, akiwa katika hali hiyo akamuhusia mtoto wake Hassan Almujtaba (a.s).

Muda wote wa siku tatu, Imamu (a.s) alikua anamtaja Mwenyezi Mungu wakati wote na kusema, nimeridhia kwa hukumu yako. Amani iwe juu ya Ali kiongozi wa waumini siku aliyo zaliwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na siku aliyo uwawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na siku atakayo fufuliwa kuwa hai kwa idhini ya Mwenyezi Mungu..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: