Kuanza (shindano la Baraaim) la kusoma surat Faat-ha kwa usahihi

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule imetangaza kuanza kwa (shindano la Baraaim) la kujifunza na kusoma surat Faat-ha kwa usahihi, kwa kutumia filamu maalumu ya katuni inayo fundisha sura hiyo (Alhamdu na Alqamaru) iliyo zinduliwa hivi karibuni.

Kiongozi wa idara ya mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano linalenga kufundisha usomaji wa surat Fat-ha kupitia filamu na kutambulisha (Alhamdu na Alqamaru), baada ya hapo tunaonyesha makosa maarufu ambayo watu wengu hukosea na kuyasahihisha kupitia ujumbe wa sauti ya kisomo cha sura hiyo utakao tumwa kwenye (telegram) kupitia namba hii: 07602306524”.

Akaongeza kuwa: “Mshiriki atume majina yake matatu pamoja na wasifu wake kimasomo na mkoa anaoishi na namba yake ya simu, tutaendelea kupokea hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu, mshiriki anatakiwa kuwa:

  • - Umri wake chini ya miaka (15).
  • - Sauti ya kueleweka.
  • - Asome taratibu sio harakaharaka.
  • - Ujumbe wa sauti atakao tuma usizidi dakika moja.

Iwapo kutakuwa na majibu sahihi mengi yaliyo timiza masharti itapigwa kura ili kumpata mshindi, tumeandaa zawadi za pesa na vitu vingine”.

Kumbuka kuwa filamu ya (Alhamdu na Alqamaru) ni filamu ya aina yake (2D), nayo ni kazi ya kwanza ya ufundishaji wa usomaji sahihi wa surat Fat-ha, imeandaliwa na wataalamu wa kituo cha uchoraji chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: